Umuhimu wa Kutangaza Mtandaoni

Online-Advertising-01-1200x638
Read Time1 Minute, 56 Second
Katika utangazaji wa bidhaa au huduma njia maarufu zilizozoeleka ni kutangaza katika Televisheni, Radio, Posta, Vipeperushi na kadhalika. Lakini Matangazo ya mtandaoni yana ufanisi mkubwa kuliko mengine iwapo yatafanywa kwa usahihi. Ufuatao ni umuhimu wa kutangaza mtandaoni.

 

1.Tangazo linaweza kupimwa ufanisi.

Tangazo lililotangazwa mtandaoni linapimika kama ni watu wangapi limewafikia na kwa muda gani na sehemu gani. Kwa mfano unaweza kujua Tangazo langu limewafikia watu 5000 ndani ya masaa 6 katika mkoa wa Dar Es Salaam. Hakuna aina nyingine ya matangazo inayoweza kukupatia taarifa hizi.

2. Gharama za Matangazo zinaendana na ufanisi wa Tangazo.

Kwa mfano kadri unavyoongeza pesa (budget) ya Tangazo ndivyo tangazo lako linavyoweza kuwafikia watu wengi zaidi. Wakati matangazo ya Radioni au kwenye TV hata ukaongeza pesa utaongeza muda tu na sio idadi ya watu.

3. Unaweza Kujenga Brand ya Biashara Yako kwa haraka.

Kwa mfano unaweza ukaanzisha Kampuni leo na ndani ya siku tatu tu Kampuni yako ikawa imejulikana Tanzania mzima. Vitu vinavyosaidia kujenga Brand Mtandaoni ni Website au Blog, Facebook Page, Au mitandao mingine ya kijamii.

4. Matangazo ya Mtandaoni yanatoa taarifa zaidi kuhusu bidhaa au huduma unayotoa kuliko matangazo yasiyo ya mtandao.

Kupitia Website au Blog unaweza kutoa taarifa kamili za Bidhaa unazouza au huduma unazotoa kwa undani zaidi, kwa makala au picha au Video na hata vyote.

5. Tangazo linaweza kuonekana kwa uhuru na kwa muda wowote mtu anaotaka.

Si kama matangazo ya radio na televisheni ambayo mtu akikosa kusikiliza wakati wa tangazo ndio tangazo lishampita. Wakati Tangazo la Mtandaoni mtua anaweza kuliona muda wowote kupitia Simu au Kompyuta yake.

6. Hayana ukomo wa mipaka.

Matangazo ya Mtandaoni hayana mipaka yaani ni wewe tu unaamuaje, hata kama unataka tangazo lako lionekane Dunia nzima litaonekana. Wakati matangazo ya tv, radio na vipeperushi au mabango linaonekana ndani ya mipaka yake tu, Kwa mfano Tanzania Tu.

7. Matangazo ya mtandaoni yanadhibitika kwa kiasi kikubwa kuliko matangazo mengine ya Biashara.

Mfano, unaweza ukaamua kuwa “Tangazo langu nataka lionekane na wanawake tu, au lionekane na watu wa Mkoa fulani tu au lionekane na Watumiaji wa simu tu au lionekane na Watu wa Wilaya fulani tu au lionekane na vijana tu, itategemea na malengo yako”.

8. Tafiti zilizofanywa hivi karibuni [Linkedin]
zinaoinyesha kwamba zaidi ya 70% ya watumiaji wa internet wanaamini kwamba Matangazo ya Mtandaoni yanategemewa sana kuliko aina nyingine yoyote ya Matangazo.

0 0
Happy
Happy
0 %
Sad
Sad
0 %
Excited
Excited
0 %
Sleppy
Sleppy
0 %
Angry
Angry
0 %
Surprise
Surprise
0 %

One Comment

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *